Kamanda wa polisi Mkoa wa Geita Kamishina msaidizi wa polisi Joseph Konyo.
Siku
chache baada ya mkuu wa polisi wilaya ya Geita Mrakibu mwandamizi wa
polisi Sadock Busee Bwire kuangusha gari la polisi PT 1998 alilokuwa
analiendesha,na kuamriwa na Kamanda wa polisi Mkoa wa Geita Kamishina
msaidizi wa polisi Joseph Konyo alitengeneze kwa pesa zake kwa madai kuwa kwa cheo chake hatakiwi kuendesha gari la polisi.
OCD
Bwire ameanza kutembeza bakuli kwa wakuu wa vituo vya nje wilayani
Geita akiwataka kila mkuu wa kituo kuchangia fedha kiasi cha
Tsh.150,000/= kwa ajili ya matengenezo ya gari hilo ambalo inasemekana
imeharibika engine yake
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakuu wa vituo vya
Butundwe,Katoro,Mgusu,Nyarugusu,Kasamwa,Lwamgasa,Nyamboge,Nzera,na
Nyakagwe wamelalamikia hatua hiyo ya Ocd kuwaamuru kuchangia gharama za
matengenezo ya gari hilo
“huyu
ocd wetu simuelewi anatuambia tuchangie hela sisi tunapata wapi?au ndio
kusema anatuagiza tuwaonee wananchi ili tupate hela ya kumpa? Alihoji
mmoja wa wakuu wa vituo
Awali
akizungumzia ajali hiyo Kamanda Konyo alisema Ajali hiyo ilitokea Mei 7
mwaka huu usiku saa 2 katika kijiji cha Bufunda tarafa ya Busanda ikiwa
imebeba watuhumiwa wa makosa mbalimbali huku
baadhi ya watuhumiwa wakitoroka,chanzo cha ajali hiyo licha ya kufichwa
imeelezwa kuwa ni mwendo kasi wa dereva wa gari hiyo.
Aliwataja
watuhumiwa waliotoroka kuwa ni William Michael,Charles Julius,Mussa
Mashiri,Joseph John,Nelson Raphael,na Sued Omary wote wakazi wa
Nyarugusu.
Aidha
Kamanda Konyo alisema kuwa kwa mujibu wa kanuni na sheria za polisi
“Police General Order” mkuu wa polisi wa wilaya ana dereva wake
haruhusiwi kuendesha gari la polisi isipokuwa la kwake binafsi.
Aliongeza
kuwa askari mmoja kati ya watatu aliyejulikana kwa jina la Konstebo
Linus wa kituo cha polisi Nyarugusu alijeruhiwa baada ya meno yake
mawili kung’oka na kulazwa katika hospitali ya wilaya kwa matibabu.
Kaimu mganga mkuu wa hospitali ya wilaya Dk.Adam Sijaona alikiri kulazwa kwa askari huyo na kudai hali yake inaendelea vizuri.
Aidha
askari polisi wa kituo kikuu cha Geita wamekuwa wakimtuhumu mkuu wa
polisi huyo wa wilaya kwa madai kuwa anashirikiana na wafanyabiashara wa
magendo hasa wa mkaa,na pombe kali aina ya viroba zinazoingizwa kinyume
nchini kutoka nchini Uganda.
Wamedai
kuwa baada ya kuwakamata wafanyabiashara hao ambao ni maswahiba wa Ocd
wakisafirisha magendo na kuwafikisha mahakamani,Ocd huyo ameamua
kuwachongea uhamisho na kupelekwa wilaya za Nyang’wale Chato na
Mbogwe,uhamisho ambao wameuita ni wa fitina wala sio wa haki.
Wameeleza
kuwa licha ya gari ya polisi kuangushwa na kuharibiwa hakuna jalada
lililofunguliwa kituoni hapo na haikukaguliwa na mkaguzi wa magari kama
taratibu zinavyoelekeza na badala yake ilifichwa kwenye gereji bubu ili
kuficha ukweli,hali ambayo imezua hofu kwa askari aliyeumia kuwa atakosa
haki zake .
Jitihada za kumpata mkuu wa polisi wa wilaya Sadock Busse Bwire kujibu
tuhuma zinazomkabili hazikuzaa matunda,baada ya simu yake kuita kwa
muda mrefu bila kupokelewa,na alipotumiwa ujumbe wa maneno hakujibu.
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Kamishina
msaidizi wa polisi Joseph Konyo alipoulizwa hatua ya wakuu wa vituo
kuamriwa kuchangia gharama za matengenezo ya gari hiyo,alidai
hawalazimishwi na wala hakuna sheria inayowabana wasipochangia,alidai kuwa analifuatilia suala hilo na baada ya hapo atalitolea ufafanuzi.
Na Valence Robert wa Malunde1 Blog- Geita