George Tyson enzi za uhai wake.
NI pigo tena kwa tasnia ya Bongo Muvi, mwongozi filamu Bongo na aliyekuwa mume wa staa wa filamu za Kibongo, Yvonny Cherry 'Monalisa',
George Tyson amefariki dunia baada ya kupata ajali mbaya ya gari maeneo
ya Gairo, Morogoro akitokea mkoani Dodoma.
Tyson alikuwa ameambatana na
watu kadhaa katika safari hiyo ambao wanadaiwa kuumia vibaya. Mwili wa
marehemu Tyson pamoja na majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa Hospitali ya
Mkoa wa Morogoro. Tyson enzi za penzi lake na Monalisa walifanikiwa
kupata mtoto aitwaye Sonia.
MUNGU AIPUMZISHE ROHO YA MPENDWA WETU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!