Kwa
mujibu wa chombo chetu cha habari kutoka Bungeni Dodoma kinasema
wabunge wa upinzani wametoka Bungeni kwa kuigomea Wizara ya Nishati na
Madini ambayo ilikuwa inapitisha bajeti yake leo. Wabunge hao wametoka
bungeni humo kwa kutotaka kushirikishwa kwenye upitishwaji wa bajeti
hiyo kwani kila mwaka haitoi utatuzi kwenye suala la Umeme na Madini ya
hapa nchini. Pia Mh. Mbowe alisema wizara hii ni kubwa inabidi igawanywe
ili uwepo ufanisi kwatika wizara hii pia ameongezea kwa kusema muda
uliowekwa wa kujadili wizara hii ni mdogo kwani wizara hii ya Nichati na
Madini ni kubwa ukilinganisha na muda uliowekwa.
Wabunge wa upinzani wakiwa wanatoka nje ya Bunge baada ya kususia kikao
Wabunge wa upinzani wakiwa wanatoka nje ya Bunge baada ya kususia kikao