MTOTO AREJESHA NDOA YA BOB JUNIOR NA MKEWE

Stori: Chande Abdallah
MTOTO wa msanii wa Bongo Fleva, Raheem Nanji ‘Bob Junior’ ametajwa kuwa ndiyo sababu kubwa ya kurejesha ndoa iliyovunjika ya msanii huyo na aliyekuwa mkewe iliyovunjika miezi michache iliyopita.

Akizungumza na mwandishi wetu, msanii huyo alisema kuwa kipindi chote wakati ameachana na mkewe alikuwa akimkumbuka sana mwanaye ambaye alikuwa akiishi na mama yake, Halima.
Raheem Nanji ‘Bob Junior’ akiwa na mwanaye.

“Wakati nimetengana na mke wangu kitu kikubwa nilichokuwa nikikimisi kilikuwa ni uwepo wa mwanangu, nashukuru Mungu kwa sasa nimerudiana naye,” alisema Bob Juniour.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo