Kwenye magazeti ya April 30 2014 Tanzania miongoni mwa stori kubwa ilikua ni hii ya kukamatwa kwa gari la kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni ambae pia ni mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe ambapo baadhi ya vichwa vya habari vilisema ni kutokana na kuhisiwa kutumika kwa ugaidi.
Mtangazaji Millard Ayo amepata nafasi ya kuzungumza na msemaji wa Polisi nchini Kenya
Gatiri Mboroki anaethibitisha kwamba ni kweli gari la Mbowe lilikamatwa
tarehe 25 April 2014 ambapo gari hilo baada ya kuvuka mpaka kuingia
Kenya likitokea Tanzania lilibadilishwa namba.
Anasema kutokana na visa vya ugaidi nchini Kenya baada ya Wananchi
kuona gari imebadilishwa namba na kupaki kwenye hoteli wakaripoti
Polisi, Polisi walikwenda na kumkuta dereva peke yake aliewaambia kwamba
kiongozi wa chama ambae ni Freeman mwenye gari amekwenda Nairobi kwa
ndege, hiyo ilileta utata kidogo kwa kujiuliza amekwenda Nairobi kwa
ndege iweje aache gari?’
Baada ya hapo gari lilipelekwa kwenye kituo cha polisi na Mh. Mbowe
akaambiwa aende kujitambulisha ambapo kweli alifika kituoni na
kujitambulisha akiwa na Mh. Wenje na baada ya hapo waliruhusiwa na
kupewa gari wakaondoka muda mfupi baadae
Kwa kumalizia Gatiri Mboroki amesema hakuna aliefungwa wala gari hilo
halijawahi kutumika kwenye visa vya ugaidi nchini Kenya na wala
halikuzuiliwa isipokua sababu pekee ya gari hilo kupelekwa Polisi ni
baada ya kuonekana likibadilishwa namba.

