LULU AIOMBA BASATA NA MAMLAKA HUSIKA ZIWARUHUSU WAIGIZE NUSU UCHI ILI KUENDANA NA SOKO LA KIMATAIFA

DIVA wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameziomba mamlaka zinazosimamia maadili ya filamu nchini ziwaruhusu wasanii waigize nusu uchi  ili kuendana na soko la kimataifa. 
 
Akitetea hoja yake mbele ya mwandishi wetu, staa huyo aliyeitendea haki filamu ya Foolish Age alitolea mfano Tamthiliya ya Shuga iliyomtoa Lupita Nyong’o ambayo alicheza akiwa nusu utupu.
 
“Wanasema hatufuati maadili wakati kuna muvi ambazo zipo theatre na watu wanaangalia hazina maadili, wao wanataka tufanye vitu kwa kudanganya wakati sasa hivi tuko dunia ambayo tuna takiwa tuweke vitu wazi, wasibane sana,” alisema Lulu.

>>GPL


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo