Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na baadhi ya Wananchi
alipokuwa akiwasili mjini Igunga,kabla ya kuzindua mradi wa Vijana
Saccos wa mjini humo mkoano Tabora.
Katibu MKuu wa CCM,Ndugu Kinana akikata utepe kuashiria uzinduzi wa wakala
wa uuzaji wa matrekta kwa wanavikundi,yanayouzwa na Vijana SACCOS
LTD,ya Igunga,inayojumuisha vikundi mbalimbali vya wilaya hiyo,wakati wa
ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali
pamoja na wananchi wilayani humo,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya
Igunga,Mh.Elibariki Kingu.
Ndugu Kinana akiwasha moja ya trekta mara baada ya kuuzindua uwakala wa zana za kilimo wa Vijana SACCOS LTD wilayani humo.
Sehemu ya wananchi walikuwa wakishuhudia uzinduzi wa wakala
wa uuzaji wa matrekta kwa wanavikundi,yanayouzwa na Vijana SACCOS
LTD,ya Igunga,inayojumuisha vikundi mbalimbali vya wilaya hiyo



