BABA wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kanumba amemshutumu mzazi
mwenziye, Flora Mtegoha, kuwa amekuwa na tabia endelevu ya kumtenga
kwenye shughuli za mwanaye.
Akipiga stori na waandishi wetu, alisema anamshangaa mama huyo
kumtenga mara kwa mara katika ishu za marehemu mwanaye ambapo alitolea
mfano wa maadhimisho ya miaka miwili ya kifo cha mwanaye (Kanumba Day)
yaliyofanyika hivi karibuni.
“Huenda wana maslahi yao kuamua kulitumia jina la mwanangu, siwezi
kuwazuia lakini watambue kuwa wanakosea sana kwa kufanya hivyo bila
kunishirikisha mimi baba yake,” alisema baba Kanumba.
VIA GPL