HUYU NDIYE MCHUNGAJI MBAKAJI, AMEMBAKA BINTI WA MIAKA 13 JIKONI


KUDADADEKI ….Mbwadidi la Wachungaji kutafuna Kondoo wao katika makanisa yao, limeibuka Upya, baada ya kuzima kwa Muda Kadhaa.
 
 Mchungaji TYRONE BANKS mwenye Umri wa Miaka 58, amewekwa Chini ya Ulinzi na kutupwa nyuma ya Nondo, baada ya Kupatikana na hatia ya Kumbaka Binti wa Miaka 13 (Jina tumelihifadhi), ambaye anatokea katika familia Rafiki.

Ripoti imezidi kumiminika kuwa, Pastor Huyo kutoka Huko ALABAMA, alikuwa ameshajijengea Uaminifu kwa Binti huyo, lakini alikuja kuharibu baada ya kutekeleza kitendo hicho kibaya kilichosababisha madhara kwa binti huyo.

Aidha Story kamili ni Kwamba, Pastor Tayrone, alimchukua Binti huyo katika gari lake, na kuenda naye katika kanisa Linalofahamika kwa jina la HUEYTOWN. Baada ya kufika huko, Mchungaji huyo alimshawishi  Binti huyo waingie Ndani, na Baada ya Kuingia tu, Alifunga Mlango kwa Funguo, na Kutekeleza tukio hilo Kinyume na Kazi yake, Heshima yake, Hadhi yake, pamoja na Sheria.

Baada tu ya Binti huyo kurudishwa Nyumbani, Moja kwa Moja alimuambia mama ake kilichotokea, huku akithibitisha kuwa alifanyiwa kitendo hicho cha Kinyama Katika Maeneo ya jikoni , ndani ya kanisa hilo.

Mpaka hivi sasa, Mchungaji Tyrone amefunguliwa mashitaka ya UBAKAJI, na yuko Mikononi mwa Polisi. 

VIA BLACK TOUCHEZ


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo