Mwimbaji nyota wa muziki wa dansi, Mwinjuma Muumin.
MWIMBAJI nyota wa muziki wa dansi, Mwinjuma Muumin amezikosoa tuzo
tatu za muziki wa dansi zilizotolewa Jumamosi, Mlimani City katika usiku
wa tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards.
Muumin alitoa tathmini yake jana mchana katika ofisi za
Saluti5 ambapo alisema hakubaliani na Mashujaa Band kupewa tuzo ya bendi
bora ya mwaka, hakubaliani pia na Jose Mara kuwa mwimbaji bora wa mwaka
huku pia akishangaa Ferguson kuwa rapa bora wa mwaka.
Mwimbaji huyo ameshangaa bendi kama FM Academia au Twanga
Pepeta kukosa tuzo ya bendi bora, lakini akashangaa zaidi Jose Mara
anakuwaje mwimbaji bora mbele ya mtu kama Christian Bella halafu
Ferguson ampiku Totoo ze Bingwa au Kitokololo.
CHANZO SALUTI5
