Staa katika tasnia ya filamu Alice Bagenzi “Rayuu” amefunguka na kusema amechoka maisha ya kuishi kiupweke hivyo anatafuta mwanaume wa kumuoa ili naye awe katika ndoa na aachane na maisha ya ukapera maana kwa sasa yanamuelemea na kila aonapo watu walio olewa jinsi wanavyoishi na wanaume zao basi na yeye anatamani sana maisha hayo.
"Natafuta mwanaume wa kuniweka ndani ambaye
atakuwa mkweli na atanipenda kwani nimechoka maisha ya kisela, nataka niwe
mke halali wa mtu tena mwanaume atakayekuja kwangu nitampenda sana” Alifunguka mbele ya Mpekuzi wetu na kuongeza:
"Mimi ni binti mzuri tena bado mdogo hivyo maisha ya kurukaruka nimechoka"
