DEREVA WA GARI LA WAGONJWA AFIA GESTI SINGIDA, MWILI WAKE WAKUTWA UKIWA NUSU UTUPU


TUKIO hili la kusikitisha lilitokea jana majira ya saa kumi na moja jioni katika Gest moja iitwayo TOP LIFE mkabala na shule ya Kiomboi Bomani mkoani Singida.
Mwili wa marehemu ambaye alikuwa ni dereva wa Gari la Hospital ya wilaya ya Iramba, Jina limehifadhiwa.
Mwili ulikutwa ukiwa umevimba ukiwa nusu utupu na pensi tu, Nguo zingine hazikujulikana zilipo.
Aidha iligundulika kuwa Dereva huyo alifariki siku mbili nyuma maana alikuwa akitafutwa na waajiri wake wa kazi bila mafanikio.
Wahudumu wa Gest hiyo walidai kuwa mlango ulifungwa na kufuli kwa nje wakawa na matumaini kuwa marehemu angerudi.
UZEMBE

Polisi walipodai daftari la wageni hawakuweza kuliona jina la marehemu, Kitu ambacho kilidhihirisha kuwa marehemu aliingia humo katika Gest hiyo kuchetua mda mchache tu (Shot Time) yani good time na sio kulala.
  Imeripotiwa na David Mtengile Singida.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo