BREAKING NEWS: TIMU YA TAIFA YA NETIBOLI YATIA AIBU BAADA YA KUINGIA UWANJANI BILA JEZI...!!!!

Wachezaji wa jiji la Mombasa walipasha weeeee!!! Wenzao Dar Es Salaam walikuwa wakisubiri jezi…..
========

Timu hiyo ni mwenyeji wa michezo ya mashindano ya mpira wa kikapu kwa majiji ya Afrika Mashariki na Kati ina ratiba ya kucheza dhidi ya Kampala.

Hata hivyo alitokea msamaria mwenye duka la vifaa vya michezo kufunika aibu hiyo kutokana na wageni kuwa wameshaingia uwanjani, na timu pinzani kupasha misuli mpaka wakachoka. Mechi ikaanza na kuendelea.

Haikuweza kueleweka mara moja sababu za timu kupelekwa uwanjani pasipo jezi hizo ambazo ni kwa mujibu wa sheria za mashindano ya kimataifa lazima zitumike.

Viongozi wa chama cha kikapu Dar Es Salaam walionekana kuhaha huku wakitokwa jasho kwa kero hiyo iliyokuwa ikiwachungulia usoni.

Hata hivyo viongozi hao hawakuweza kupatikana kuzungumzia heka heka hiyo.

>>>Taarifa news


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo