Na Martha Mboma. BEKI wa Coastal
Union, Abdi Banda, amefunguka na kusema yupo katika hatua nzuri ya
kuweza kumalizana na Yanga, huku akiwa anavunja mkataba wake.
Beki wa Coastal Union, Abdi Banda.
Kabla ya msimu uliopita Yanga ilikuwa ikimhitaji beki huyo ambaye
alipandishwa kutoka timu ya vijana ya Coastal na kuweza kuchezea timu
kubwa lakini aliwatolea nje.
Akizungumza na Championi Jumatano, beki huyo alisema
kwa sasa yuko katika mazungumzo mazuri na Yanga kwa ajili ya kuungana
nao kwa msimu ujao na anavunja mkataba na timu yake.
Banda alisema ameamua kujiungana na timu nyingine na anatarajia kuvunja mkataba na Coastal japo sababu za kuvunja hajaziweka wazi na kukiri kuwa mazungumzo yapo katika hatua nzuri.
“Kwa sasa nipo katika mazungumzo na Yanga na tumefika pazuri, suala
la kuendelea kuitumikia Coastal Union halipo kwa sababu natarajia
kuvunja nao mkataba ili niweze kuendelea na mambo yangu.
“Yanga walikuwa wakinihitaji kwa muda mrefu lakini tukikubaliana na tumefika pazuri, nipo tayari kwenda kuitumikia na si kurudi Coastal ingawa sipo tayari kusema ni kitu gani kimenifanya niondoke kule,” alisema Banda.
Japo kwa upande wa Coastal Union hali si shwari kumekuwa na migogoro
baina ya viongozi huku wachezaji wengi wakiripotiwa kuondoka na hata
kuvunja mikataba yao kutokana na kutokuwepo kwa maelewano mazuri ndani
ya klabu.
>>>Championi Jumatano
