Watu wawili wamefariki dunia kwa kujinyonga katika matukio yaliyotokea nyakati tofauti wilayani Makete mkoani Njombe huku matukio hayo yakishabihiana kwa kiasi fulani
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na ofisi ya mkuu wa polisi wilayani Makete hii leo imesema katika tukio la kwanza Bi Anamaria Mahenge aligundua kujinyonga hadi kufa kwa Paul Mbilinyi ambaye alijinyonga kwa kutumia kitambaa cha wanawake cha kujifungia Kichwani
Tukio hilo limetokea Aprili 30 mwaka huu majira ya saa mbili asubuhi katika kijiji cha Ivalalila kata ya Iwawa wilayani hapa
Aidha taarifa hiyo imesema katika tukio la pili jeshi hilo lilipokea taarifa ya kujinyonga hadi kufa kwa Fonzina Israel Msigwa ambaye naye alijinyonga kwa kutumia kitambaa cha kujifunga kichwani cha wanawake
Tukio hilo lilitokea Mei 4 mwaka huu majira ya saa tano kamili usiku huko katika kijiji cha Ibaga kata ya Mang'oto wilayani hapa
Matukio hayo licha ya kutokea katika vijiji tofauti yanafanana kwani wote waliofariki walijinyonga kwa kutumia kitambaa cha kujifunga kichwani cha wanawake.
