SHULE MPYA YA SEKONDARI YA MAKETE GIRLS YAANZA KUPOKEA WANAFUNZI

Zoezi la kupeleka wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari Makete Girls, linaendelea vizuri na tayari wanafunzi na waalimu wamesharipoti shuleni hapo. 

Akitoa taarifa ya awali kwa mwandishi wa habari hizi Diwani wa kata ya Ukwama ilipo shule hiyo Bw. Smith Sanga amesema kama ilivyoahidiwa hivi karibuni na serikali kuwa shule hiyo itaanza kupokea wanafunzi ndani ya mwezi Aprili imetekelezeka jambo linalowafurahisha wananchi wa kata yake ambao walishirikiana na serikali kuijenga shule hiyo.

 Amesema shule hiyo ya pekee ya wasichana wilayani Makete mkoani Njombe inategemewa kuwa sekondari ya mfano, hivyo kutoa wito kwa wananchi na viongozi mbalimbali kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha wanafunzi wanaosoma na watakaokuja kusoma shuleni hapo wanapata elimu iliyobora kuwawzesha wafaulu vizuri. 

Katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika kwa siku mbili mfululizo (Alhamisi na Ijumaa) wakatia akisoma taarifa ya kata yake diwani huyo alisema zoezi la kuwapeleka wanafunzi katika shule hiyo linaendelea na tarayi imekwishaanza kazi kama serikali ilivyoahidi. 

Ujenzi wa shule hiyo ni jitihada za watu mbalimbali akiwemo Mkuu wa wilaya ya Makete mh Josephine Matiro, wazawa wa Makete ambao wanaishi nje ya wilaya hiyo, wananchi wa kata ya Ukwama, serikali pamoja na wadau mbalimbali ambao kwa pamoja walijitoa kuhakikisha shule hio inajengwa


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo