WAKAZI WA ISAPULANO MAKETE WATEMBEA UMBALI MREFU KUFUATA USAFIRI WA BASI

Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha wilayani Makete na kupelekea uharibifu wa baadhi ya barabara ikiwemo ya Isapulano na kusababisha magari kupita kwa tabu na mengine kukwepa barabara hiyo, Afisa mtendaji wa kata amezungumzia sakata hilo. 

Afisa mtendaji huyo Bw. Alimivu sanga amesema wanadhani huwenda eneo hilo lina chemchem ya maji kwa kuwa wameshajaribu kufukia shimo hilo kwa mawe makubwa lakini baada ya muda mchache mawe hayo yamezama na hapaoneshi kama palifukiwa kwa mawe. 

Amesema kwa sasa wameshaomba wadau kujitolea magari yao ili kwenda kusomba mawe na kifusi cha kufukia hapo lakini bado wanahofu kuwa kazi hiyo ni sawa na bure. 

"Mimi ninadhani huwenda hapa chini kuna chemchem ama mkondo wa maji, na hivi sasa kwa jinsi mvua inavyonyesha ndio panazidi kuharibika, nahisi panahitaji utaalamu wa kina" alisema. 

Kufuatia mabasi ya abiria kuacha kupita kijijini hapo kutokana na ubovu wa barabara hiyo, wananchi hao hulazimika kutembea kwa miguu zaidi ya kilomita mbili hadi kwenye makutano ya barabara ya Ivalalila na Ujuni katika kijiji cha Nkenja ili kupanda basi kwa ajili ya kwenda mkoa jirani wa Mbeya. 

Hata hivyo kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha haziruhusu kukarabatiwa kwa barabara hadi hapo zitakapomalizika mwishoni mwa mwezi Mei ama Juni mwanzoni.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo