KATIKA hali ya kushangaza na kusikitisha, askari polisi Raphael
Maganga, juzi aliibiwa pikipiki yake aliyokuwa ameiegesha ndani ya
Uwanja wa Taifa wakati wa mechi ya kirafiki kati ya Taifa Stars na
Burundi.
Mechi hiyo ya kirafiki iliyomalizika kwa Stars kukubali kichapo cha
mabao 3-0, ilitazamwa na mashabiki bure baada ya kudaiwa Rais Jakaya
Kikwete aliamuru waingie bure ili waipe sapoti timu hiyo.
Akizungumza kwa masikitiko mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo,
Maganga akiwa ameshika funguo zake mkononi, alisema haamini
kilichotokea, kwani anaona kama ‘movie’.
Maganga alisema pikipiki yake yenye namba za usajili T 454 CUP, aina
ya Fekon, aliipaki upande wa kulia wa uwanja na baada ya mechi
kumalizika hakuikuta.
Alisema ameshafungua jalada lenye namba CHA/RB/36665/2014 Kituo cha Polisi Chang’ombe.
Na
Clezencia Tryphone