PROF. LIPUMBA AKATAA UTEUZI WA KAMATI YA UONGOZI BUNGE LA KANUNI

Na Magreth Kinabo, Maelezo Dodoma  
 
MWENYEKITI wa Bunge Maalum la Katiba, Samwel Sitta, ametangaza majina ya wenyeviti na makamu wenyeviti wa Kamati za bunge hilo. Majina hayo yametangazwa na Mwenyekiti huyo baada ya uchaguzi wa viongozi hao uliofanyika Machi 24, 2014 mjini hapa.

Mwenyekiti huyo aliyataja majina hayo katika Kamati ya Uandishi Mwenyekiti, Andrew Chenge, Makamu wake ni Mgeni Hassan Juma. Kamati ya Kanuni Mwenyekiti ni Pandu Ameri Kificho, Makamu wake ni Dk. Susan Kolimba. Kamati Na. 1 Mwenyekiti ni Ummy Ally Mwalimu, na Makamu wake ni Prof. Makame Mbalawa.

Wengine waliochaguliwa katika Kamati Na. 2 Mwenyekiti ni Shamsi Vuai Nahodha, Makamu wake ni Shamsa Mwangunga. Kamati Na. 3 Mwenyekiti ni Dk. Francis Michael, Makamu wake ni Fatma Mussa Juma.

Sitta alisema waliochaguliwa katika Kamati Na. 4 Mwenyekiti ni Christopher Ole-Sendeka, Makamu wake ni Dk. Sira Ubwa Mamboya, Kamati Na. 5 Mwenyekiti ni Hamad Rashid Mohamed Makamu wake ni Assumpter Mshama.

Viongozi waliochaguliwa katika Kamati Na. 6 Mwenyekiti Stephen Wassira na Makamu wake ni Dk. Maua Daftari. Kamati Na. 7 Mwenyekiti Brig. Hassan Ngwilizi, Makamu wake Waride Bakari Jabu. Kamati Na. 8 Mwenyekiti ni Job Ndugai, Makamu wake ni Biubwa Yahya Othman.

Kamati Na. 9 Mwenyekiti ni Kidawa Hamidi Saleh, Makamu wake Wiliam Ngeleja, Kamati Na. 10 Mwenyekiti ni Anna Abdallah, Makamu wake ni Salmin Awadh Salmin. Kamati Na. 11 Mwenyekiti ni  Anne Malecela, Makamu wake Hamad Masauni na Kamati Na. 12 Mwenyekiti                           Paul Kimiti na Makamu wake ni Thuwaybah E. Kisasi.

Wakati huo huo, Sitta alitangaza wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalum la Katiba, ambao ni wenyekiti na makamu wenyeviti wa kamati hizo wakiwemo wajumbe wengine watano aliowateua. Wajumbe hao walioteuliwa na Sitta kuingia katika kamati hiyo ni Fakharia Khamisi Shomari, Mary Chatanda, Profesa Ibrahim Lipumba, Amon Mpanju na Hamad Abuu Juma.

Hata hivyo pamoja na majina hayo kutangazwa Profesa Lipumba alisimama na kulalamikia upendeleo katika kamati hiyo na kudai CCM imefanya vikao hivyo kama vikao vya chama kwa kujazana viongozi wengi wa chama hicho hivyo yeye kugomea uteuzi wake.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo