KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AWASILI MKOANI RUKWA LEO TAYARI KWA KUANZA ZIARA YAKE YA SIKU 21



 Ndege iliyombeba Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana ikiwasili katika uwanja wa ndege mjini Sumbawanga,mkoani Rukwa mchana huu. 


 Ndugu Kinana akishuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili mchana huu Sumbawanga mkoani Rukwa,tayari kwa kuanza ziara yake rasmi mkoni humu,ambapo ziara yake rasmi inaanzia Wilaya ya Nkasi,mkoani Rukwa.


 Ndugu Kinana akipokelewa na viongozi mbalimbali wa CCM mkoa Rukwa mara baada ya kuwasilia mapema leo mchana.


 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akivalishwa skafu na vijana wa chipukizi mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege mjini Sumbawanga,mkoani Rukwa mapema mchana huu.


Katikubu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Kada maarufu wa CCM,Ndugu Chrisant Mzindakaya,mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege mjini Sumbawanga,mkoani Rukwa mapema mchana huu.Kinana amewasili mkaoni humu mapema leo mchana ambapo anatarajia kuanza ziara yake rasmi ya siku 21 wilayani Nkasi,mkoani humo.


Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwasalimia wananchi na wanachama mbalimbali wa CCM waliofika uwanja ndege mjini Sumbawanga kumpokea mapema leo mchana.Kinana amewasili mkoani humu mapema leo mchana ambapo anatarajia kuanza ziara yake rasmi ya siku 21 wilayani Nkasi leo,mkoani humo ikiwemo mkoa wa Katavi na Kigoma..
 Baadhi ya Wananchi na wanachama mbalimbali wakisubiri kumpokea katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana kabla ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege mjini Sumbawanga mkoani Rukwa mapema leo asubuhi.


 Ni Chungu lakini kinatumika kama ngoma kikiwa kimebebwa baada ya kazi yake kuisha wakati wa kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kina mapema leo mchana mjini Sumbawanga.


Msafara wa Katibu Mkuu,Ndugu Kinana ukiondoka uwnaja wa ndege mjini Sumbawanga mapema leo ukielekea wilayani Nkasi kuanza rasmi ziara yake ya siku 21,ambayo itaambata na mikoa mitatau ikiwemo Katavi na Kigoma.

PICHA NA MICHUZIJR-MICHUZI MEDIA GROUP-RUKWA.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo