ELIMU YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE JUU YA UFUGAJI NYUKI YAANZA KUFANYIWA KAZI KWA VITENDO

 Baadhi ya Mizinga ya Nyuki katika Kikundi cha Mshikamano Katika Kijiji cha Iyayi Wilayani Wanging'ombe

Na Gabriel Kilamlya Wanging'ombe
Wanachama wa Kikundi cha Ufugaji Nyuki cha Mshikamano Kilichopo Katika Kijiji cha Iyayi Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe  Kimetajwa Kukabiliwa na Uhaba wa Mtaji wa Kuongeza Mizinga Ya Nyuki Ili Iweze Kufikia Mizinga Mia Tano.

Hadi Sasa Kikundi Hicho Kimefanikiwa Kumiliki Mizinga 225  Ya Nyuki Ambayo Imetolewa na Wafadhili Katika Kuwakwamua Wananchi Kiuchumi.

Akizungumzia Hali ya Kikundi Hicho Mwenyekiti wa Kikundi Bwana S-----Sungura Amesema Kuwa  Kikundi Hicho Tangu Kianze Mwezi April 17 Mwaka 2013 Kimefanikiwa Kupa Fedha Kiasi Cha Zaidi ya Shilingi Milioni Mbili Kutokana na Mavuno Ya Asali.

Akizungumzia Suala la Ufugaji Nyuki Katika Kikundi Hicho Mkuu wa Mkoa wa Njombe Capteni Mstaafu Asseri Msangi Amewataka Wataalamu wa Nyuki Kuhakikisha Wanasaidiana na
Wananchi Katika Kuhakikisha Wanafuga Kitaalamu Ili Waweze Kupata Asali Nyingi Zaidi.

Aidha Msangi Amewashauri Wananchi Hao Kuboresha Maeneo Ya Ufugaji wa Nyuki Hao Kutokana na Hali Ya Mvua Zinazoendelea Kunyesha Ili Kuongeza Kiwango cha Uzalishaji wa Asali.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo