DIAMOND PLATNUMZ AKERWA NA BASATA KUZIONDOA NYIMBO ZA SNURA JUX NA MADEE KUGOMBEA TUZO ZA KILI 2014


Ni msanii ambaye anaweza kuwa ametajwa zaidi kwenye tuzo za KTMA 2014 lakini Diamond Platnumz hajaliacha Baraza la Sanaa Tanzania likae kwa amani kwa uonevu ilioufanya kwa Jux, Madee na Snura kutokana na kuziondoa nyimbo zao kwenye mchakato wa KTMA 2014.

Kupitia Instagram, Diamond ameandika:
 
"Ikiwa kweli tunalengo la kutoipotosha kimaadili jamii yetu na vizazi vyetu pendwa, nafikiri ni vyema tungeanza kuzuia Video na nyimbo za kutoka nje, kuliko kuzuia nyimbo na video za nyumbani ambazo uchafu wake Haufikii hata robo ya uliopo kwenye Nyimbo zinazopewa kipaumbele toka nje… 

"Hii ni sawa na kuzidi kuukuza mziki wa nje huku tukiudidimiza na kuua mziki wetu… Will the target of reaching our goals ever be achieved?? #Ni_Mtazamo_tu."


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo