Safari
hii ni Imamu wa Jumuiya ya Sawiyatu Qadiria ambaye ni mkazi wa Tindiga
eneo la Unga Ltd,jijini Arusha, Hassan Bashir (33), ambaye amemwagiwa
kimiminika kinachosadikiwa kuwa tindikali sehemu ya mabegani iliyosambaa
maeneo ya mgongoni na shavu la kushoto.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema jana kuwa tukio
hilo lilitokea juzi saa 3:45 usiku maeneo ya msitiki huo.
Hata
hivyo, Sabas alisema upelelezi kuhusiana na tukio hilo bado unaendelea
ikiwa ni pamoja na kutumia kopo lililokuwa na kimiminika hicho ambacho
kimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kujua uhalisia wake.
Alisema,
uchunguzi wa awali wa polisi umebaini kwamba muda si mrefu kabla ya
tukio hilo, Hassan, alikuwa anatokea maeneo ya kituo kikuu cha mabasi
cha Arusha baada ya kuachana na wenzake wawili ambao walikuwa wanajadili
kikao cha Maulid.
Alisema
muda huo wa saa 3:45 alikuwa maeneo ya karibu na kwake Unga Ltd, ndipo
alipomuona mtu amesimama kwenye kiambaza cha msikiti, alimsalimia,
lakini hakumbuki kama alijibiwa.
Alisema
wakati akiendelea kuelekea kwake, alihisi kuna mtu anamfuata na
alipogeuka ili ajue ni nani, ghafla mtu huyo alimwagia kimiminika
kinachosadikiwa kuwa ni tindikali.
Alisema mara baada ya kitendo hicho mtuhumiwa alikimbia na kuelekea kusikojulikana.
Alisema
baada ya taarifa hiyo polisi waliokuwa doria maeneo ya karibu
walikwenda katika eneo hilo na kukuta kopo dogo ambalo linasadikiwa kuwa
lilikuwa na kimiminika kinachosaidikiwa kuwa na tindikali.
IMAMU AZUNGUMZA
Akizungumza
kwa maumivu makali katika wodi ya wanaume majeruhi ya Hospitali ya
Mount Meru jana, Hassan, alisema tukio hilo lilitokea baada ya kumaliza
mazungumzo ya kuandaa maulidi ya msikiti mdogo wa babu yake wa Jumuiya
ya Sawiyatu Qadiria, uliopo mtaa wa Tindigani.
Anasema
wamepanga kufanya maulidi hayo Februari 16, mwaka huu na aliwataja
aliokuwa akizungumza nao kuwa ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Ismail
Olomi na Abdallah Sadila Kaduma ambaye ni mwenyekiti wa ujenzi wa
msikiti huo.
Anasema
baada ya mazungumzo hayo alianza kurejea kwake, na akapita eneo moja
lenye maduka mawili moja likiwa linauza bidhaa za Kiislamu alikutana na
mtu akiwa amesimama jirani akiwa amevaa koti lenye rangi nyeusi.
Alisema
alimsailimia, lakini hakuweza kujua kama aliitikia au la, na yeye
akaendelea na safari zake, lakini kumbe mtu huyo baadaye alimfuata kwa
nyuma na alipogeuka kumwangalia alishtukia akimwagiwa kimiminika hicho.
Akizungumzia sababu hayo ya kutendewa hivyo, Hassan alisema itakuwa ni kutokana na mgogoro wa ujenzi wa msikiti huo.
“Sijagombana
na mtu wala kurushiana maneno na mtu lakini tukio hili naweza
kulihusisha na ugomvi wa kugombea msikiti huo kati yake na jamaa mmoja
(jina linahifadhiwa) ambaye alikuwa ananitisha kwa maneno kuhusu msikiti
huo.
“Nilimwambia
huyo jamaa kwamba nipo tayari kufa, wakati fulani aliwahi kumpiga
mwanafunzi wangu (jina linahidhiwa pia) na baada ya kushtakiwa, Mahakama
ya Mwanzo ya Maromboso mwaka jana ilimfunga kifungo cha nje cha mwaka
mmoja,” alisema.
Kwa mujibu wa Kamanda Sabas, mtu mmoja anahojiwa na polisi kuhusiana na tukio hilo.
MATUKIO YA TINDIKALI
Kwa
kipindi cha miaka mitatu tangu mwaka 2012, viongozi mbalimbali wa dini
na wasichana wawili raia wa Uingereza wamemwagiwa tindikali kwa nyakati
tofauti na watu wasiojulikana.
Viongozi
hao na miezi waliyokutwa na matukio hayo ni Novemba mwaka 2012, Katibu
wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga, Mei, mwaka 2013, Sheha wa
Tumondo Mohamed Omary Said, Julai mwaka 2013, Shekhe Mkuu Wilaya ya
Arumeru, Said Juma Makamba.
Agosti
7, 2013, wafanyakazi wa kujitolea kutoka Uingereza, Katie Gee na
Kirstie Trup, walimwagiwa tindikali wakiwa eneo la Mji Mkongwe mjini
Zanzibar.
Septemba, 2013, Padri wa Parokia ya Machui ya Kanisa Katoliki Zanzibar, Anselem Mwang’amba.
CHANZO: NIPASHE
