Jeshi la polisi mkoani SINGIDA limekamata vipande 21 vya meno ya Tembo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 43.
Mtu mmoja George James amekamatwa kwa tuhuma za kukutwa na meno hayo ya tembo yakiwa yamehifadhiwa katika mabegi mawili ya kusafiria.
Mtuhumiwa
huyo alikamatwa katika kizuizi cha idara ya maliasili kilichoko katika
kijiji Ukimbu, kata ya Mgandu, wilayani Manyoni akiwa katika gari aina
ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T797CQL.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Singida RPC Geofrey Kamwela (katika video) amesema
vipande hivyo 21 vina thmani ya zaidi ya shilingi milioni 43 na vyote
vimehifadhiwa katika kituo cha polisi wilayani Itigi."Meno haya yanaashiria kuuwawa kwa tembo wanne", alisema Kamanda James.
Vitendo
vya ujangili wilayani MANYONI vimekuwa vikiongezeka ambapo mwaka 2013
askari mmoja wa jeshi polisi alipoteza maisha katika mapambano na
majangili wilayani humo.
Tukio
hili la limekuja wakati leo Rais Jakaya Mrisho Kikwete amehudhuria
mkutano maalumu wa kupambana na ujangili na biashara ya meno ya tembo na
pembe za Faru jijini London, Uingereza. Katika mkutano huo amependekeza kupigwa marufuku biashara hiyo ili kuweza kudhibiti ujangili duniani kote.
