Hapa gari hii iliyokuwa ikiendeshwa wa WP akisogezwa ili kumpakia askari mwenzao hamakamani hapo.Picha na habari kwa hisani ya Francis Godwin.
Hapa gari likisogezwa upande wa pili baada ya upande huu kuona waandishi wametanda na kamera
Hapa gari likisogezwa upande wa pili baada ya upande huu kuona waandishi wametanda na kamera
Hapa wakimsukumiza katika gari hilo
gari hilo likitoka kwa mwendo wa kasi mahakamani hapo likiwa na mtuhumiwa wa mauwaji ya Mwangosi
Mwanahabari Frank Leonard baada ya kuachiwa huru na polisi leo
.........................
WAKATI
mahakama kuu kanda ya Iringa ikianza kusikiliza kesi ya mauwaji
ya aliyekuwa mwandishi wa Chanel Ten na mwenyekiti wa chama cha
waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) marehemu Daudi Mwangosi ,polisi
mjini Iringa waanza kuwanyanyasa wanahabari wanaofika kufuatilia
kesi hiyo baada ya kumkamata mwenyekiti wao Frank Leonard akiwa ndani ya
mahakama wakati kesi hiyo ikiendelea.
Mwenyekiti
huyo alikamatwa leo majira ya saa 5 asubuhi wakati jaji Mary
Shangali akiendelea kumsikiliza wakili wa serikali Adoph Maganga
ambae alikuwa akiwasilisha baadhi ya vielelezo muhimu vya kesi hiyo
mahakamani hapo.
Hata
hivyo katika hali iliyowashangaza wananchi na wanahabari
waliofika mahakamani hapo kusikiliza kesi hiyo ni baada ya askari
mmoja kusimama ghafla katika kiti chache na kwenda kwa wakili wa
serikali na kurudi eneo ambalo wanahabari walikuwa wamekaa na
kumsimamisha Leonard na kwenda kumpeleka kituo cha polisi kwa madai
kuwa amepiga picha mahakamani hapo wakati jaji akiendelea na kesi
jambo ambalo si la kweli.
Akizungumia
uamuzi huo wa askari hao kumkamata Leonard alisema kuwa aatambua
taratibu zote za kimahakama na kuwa asingeweza kupiga picha wakati
jaji akiendelea na kesi na kuwa kilichotokea baada ya kuingia
mahakamani hapo kamera yake ilikuwa ndani ya mfuko huku yeye
akiendelea kuchukua maelezo kwa kuyaandika .
Hata
hivyo alisema wakati huo simu yake aliyokuwa ameiweka mfukoni
wakati akiitoa mfukoni na kutaka kuiweka vizuri askari huyo aligeuka
na kuona ameishika simu hiyo na hivyo kuhisi kama amepiga picha na
kumkamata na kutaka
kumbambikia kesi ya kupiga picha mahakamani ila baada ya uchunguzi
wa awali na maelezo ilibainika si kweli na ndipo alipoachiwa huru na
kutakiwa kuripoti baada ya muda kituoni hapo.
Kabla
ya kukamatwa kwa mwenyekiti huyo wa IPC wanahabari zaidi ya 10
waliokuwepo mahakamani hapa mapema majira ya saa 2 asubuhi walizuiwa
na askari polisi waliomfikisha mahakamani mtuhumiwa wa mauwaji hayo kuwa
hawapaswi kuingia mahakamani kusikiliza kesi hiyo
kabla ya kufikisha malalamiko hao kwa msajili wa
mahakama ambae alipinga hatua ya jeshi la polisi kufukuza wanahabari
mahakamani hapo.
Hatua ya polisi hao kumkamata mwanahabari huyo iliwalazimu wanahabari kumtafuta kamanda wa polisi mkoa wa Iringa kwa
njia ya simu ili kuhoji uhalali wa jeshi la polisi kuzuia
wanahabari katika mahakama hiyo na kwakesi hiyo ya askari anayetuhumiwa kufanya mauwaji ya Mwangosi.
Akizungumza
kwa njia ya simu akiwa safarini kamanda Mungi alisema polisi hawana
mamlaka ya kuwazuia wananchi ama wanahabari
wanaofika mahakamani kwani mwenye mamlaka ya kufukuza ama kuagiza
kwa mtu yeyote anayevunja sheria ndani ya mahakama kukamatwa ni
hakimu ama jaji anayesikiliza kesi na si polisi .
Hata
hivyo wanahabari hao wameeleza kusikitishwa na askari polisi hao
kuendelea kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari katika kesi hiyo ya
Mwangosi huku kesi nyingine zikiwemo za wana siasa kufikishwa
mahakamani kwa tuhuma za vurugu polisi
hao wamekuwa wakionyesha urafiki wa
hali ya juu na wanahabari na hata kuwapigia simu ili kufika
mahakamani ila inapofika kesi ya mwenzao huyo wamekuwa wakiwageuka
wanahabari na kuwaona adui .
Mtuhumiwa
huyo ambae alifikishwa mapema zaidi kuliko simu nyingine na gari la
polisi akiwa mbele aliondolewa mahakamani hapo kwa kufishwa kupita
kiasi na
kuingizwa katika gari dogo binafsi lenye namba T
165 BMP lililokuwa likiendeshwa na askari mwanamke (WP) huku vioo vya
gari hilo vikiwa haviangazi kwa ndani huku watuhumiwa wawili wa
mauwaji ambao walikuwa na askari huyo mahakamani hapo wakipakiwa
katika karandinga la polisi.
Msajili wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda
ya Iringa, Dunstan
Nduguru aliwashangaa Polisi kwa kuingia shughuli za mahakama.
"Hata
kama mwandishi huyo angekuwa anapiga picha, haikuwa kazi yao kumkamata mpaka
wapewe agizo na Jaji Mfawidhi aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo," alisema.
Pamoja
na askari hao kuwazuia wanahabari kuchukua picha mara baada ya mtuhumiwa huyo
kufikishwa mahakamani, Nduguru alisema utaratibu wa mahakama unawaruhusu
wanahabari kuchukua picha kabla shughuli kabla shughuli za mahakama hazijaanza
na baada ya shughuli hizo kwisha.