MKUTANO MKUU WA MAOFISA WAANDAMIZI WA JESHI LA POLISI WAANZA LEO MJINI MOSHI


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu, akisalimiana na makamishna wa Jeshi la Polisi baada ya kuwasili kwa ajili ya kumpokea mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya ndani kwenye ufunguzi wa mkutano Mkuu wa Maofisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika katika chuo cha taaluma ya Polisi Moshi.
Naibu waziri wa Mambo ya Ndani Mh, Pereira Ame Silima akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu baada ya kuwasili katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi kwa ajili ya kufungua mkutano Mkuu wa Maofisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika katika chuo hicho.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akitoa hotuba jana katika ukumbi wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua mkutano Mkuu wa Maofisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika katika chuo hicho.
Maofisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya ndani, Mhe. Pereira Ame Silima kwenye ufunguzi wa mkutano Mkuu wa Maofisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika katika chuo cha taaluma ya Polisi Moshi. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo