Mrembo aliyewahi kushiriki miss Tanzania Hamisa Mobeto a.k.a Hamisa kadomo amekanusha tetesi za kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii kipenzi cha kinadada Naseeb Abdul a.k.a Daimond Platnumz na kusema kuwa anamuheshimu kama shemeji yake.
Hamisa ambaye pia amewahi kuonekana katika video ya msanii Quick
Rocka ‘My baby’, ameiambia Global Publishers kuwa maneno yanayosemwa si ya kweli na wala haitawahi kutokea.
“Kamwe siwezi kutembea na Diamond na haitatokea kwani jamii nzima
inajua yupo na Wema na mimi huyo mtu ni rafiki yangu mkubwa, hana chake
hapa, siwezi kutembea naye kamwe, namheshimu kama shemeji yangu”.Alisema mrembo huyo.
Mrembo huyo ambaye uzuri wake unazidi kumpa dili kibao ndani na nje
ya Tanzania kila kukicha, ameongeza kuwa hana mazoea na staa huyo wa
‘Number One’ na kama kuonana waliwahi kuonana miaka ya nyuma na si
kimapenzi.
Source: Global Publishers
