MAKAMU WA RAIS,DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA UWEKEZAJI KANDA YA ZIWA,JIJINI MWANZA


  Mgeni Rasmi katika Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal akitoa hotuba yake wakati wa Ufunguzi wa Kongamano hilo,uliofanyika mapema leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika,Jijini Mwanza.
 Mwenyekiti wa Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Mh. George Kahama akitoa hotuba yake wakati wa Ufunguzi wa Kongamano hilo,uliofanyika mapema leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika,Jijini Mwanza.
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Evarist Ndikilo ambaye ndie Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,akizungumza na washiriki wa Kongamano hilo (hawapo pichani) wakati ufunguzi wake uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Malaika,Jijini Mwanza.
 Waziri wa Viwanda na Biashara,Mh. Abdallah Kigoda akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi kuja kuzungumza na Washiriki wa Kongamano hilo,jijini Mwanza leo.
Balozi wa Afrika ya Kusini nchini Tanzania,Mh. Thamduycse Chilliza (katikati) akifatilia Kongamano hilo sambamba na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC),Julieth Kairuki (kushoto).Kulia ni Msaidizi wa Balozi wa Afrika Kusini,Terry Govender.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo