DIWANI WA KATA YA MBWENI BONIFACE MNYACHIBE (CCM) AFARIKI DUNIA


Marehemu Boniface Mnyachibwe Enzi za Uhai wake


TANZIA.
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni inapenda kutangaza kifo cha Diwani wa kata ya Mbweni Mh. Boniface Mnyachibwe kilichotokea leo ghafla saa tatu asubuhi.

Tunatoa pole kwa familia yake, wakazi wa Mbweni, Wananchi wa Kinondoni pamoja na Chama chake cha CCM.

Mchango wake mkubwa ktk kuboresha maisha ya wakazi wa Mbweni na Kinondoni kwa kujituma na uadilifu kamwe hautasahaulika. Aidha, kifo chake cha ghafla leo wakati jana tulikuwa naye mpaka saa moja na nusu jioni kwenye vikao vya bajeti ni uthibitisho wa uzalendo wake na mapenzi yake kwa anaowawakilisha na Kinondoni kwa ujumla.
Dua zetu na sala zetu ziende kwa familia yake na wote aliokuwa anawawakilisha.
Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahala pema peponi-AMIN.
Imetolewa na Manispaa Ya Kinondoni


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo