YUNEDA MKOMBOZI WA WASANII BONGO:KUSAMBAZA MUVI YA WHY LINAH? JUMATATU HII

KAMPUNI mpya ya usambazaji wa filamu Bongo ya Yuneda Entertainment imeingia katika biashara ya usambazaji baada ya kilio cha wasanii kukosa sehemu za kuuza filamu zao au kusambaziwa, kampuni hiyo inayojali ubora kwa kazi za sinema imeingia nchini kuanza kwa kusambaza filamu ya Why Linah?

Filamu hiyo iliyoshirikisha wasanii nyota katika tasnia ya filamu Bongo kama Hemed Suleiman ‘Phd’, Rose Ndauka, Charles Magali ‘Mzee Magali’, pamoja na wasanii wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu Swahilihood, filamu hiyo inaingia leo jumatatu.

Wasanii wamefurahia sana ujio wa kampuni hiyo kwani wanaamini kuwa wengi wataweza kusambaziwa kazi zao kwani moja ya sifa hiyo ni ya kizalendo inayojali maslahi ya wasanii, na inaongozwa na wazalendo wanaojua hali halisi ya soko la filamu nchi Tanzania.

Hivyo kwa kuzingatia umakini na ubora wa filamu Yuneda Entertainment wanakuletea filamu yenye viwango vya kimataifa ya Why Linah?.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo