CHAMA
cha Mapinduzi (ccm), kimejiingiza matatani baada ya kuwapangisha
wafanyabiashara wawili katika fremu moja la kufanyia biashara.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam mfanyabishara Charles
Msigwa alisema aliingia mkataba na Mecy Mziray ambaye kwa sasa ni
marehemu na aliendelea kumlipa kodi ndugu wa marehemu Vesta Haule.
Alisema wakati akiendelea kufanya biashara katika banda hilo
alishangazwa na viongozi wa CCM tawi la Vigaeni Kata ya Ndugumbi
kumfuata wakitaka aingie mkataba upya na chama hicho.
“Nimekuwa nikiendesha shughuli zangu za biashara kwa muda wa
miaka minne ndipo nilipofuatwa na viongozi wa CCM na kunishauri nichukue
mkataba nao ili chama kipate mapato,”alisema Msigwa.
Aliongeza kuwa viongozi hao walimuita kwenye ofisi ya tawi na kumuhakikishia hakutakuwa na tatizo lolote juu ya mkataba huo.
“Viongozi hao waliniambia kuwa mabanda hayo hayarithishwi hata
hivyo aliyeachiwa amekuwa msumbufu wa kodi mwenye banda alishafariki kwa
hiyo banda huwa linarudi na kuwa mali ya chama,”alisema.
Msigwa alisema kuwa aliujaza mkataba huo na kuurudisha ofisini kwao alipotaka kuulipia akawa anazungushwa zungushwa.
“Nilipeleka malalamiko yangu Kwa uongozi wa Wilaya ambapo
uliwaandikia barua ya kwamaba wanitafutie banda jingine iwapo nikiwa
tayari kutimisha masharti ya kuwa mpangaji wa chama hicho na nilikubali
lakini uongozi huo haukufanya kama ulivyo agizwa,”alisema Msigwa.
Awali
Chama cha mapinduzi (CCM) kiliingia mkataba wa kujenga banda hilo na
Marehemu Mecy Mziray gharama zake na asingeweza kutoka mpaka gharama
zake za ujezi zitakapo malizika.