MSANII
wa filamu nchini Athumani Lali 'Budege' baada ya kucheza filamu za watu
sasa ameamua kuja na filamu zake mwenyewe na kuwawezesha wasanii wenzie
kuwa na kipato kizuri baada ya kuamua kufungua kampuni yake binafsi
inayokwenda kwa jina la AJM Entatainment ambayo ina husika na maswala ya
filamu za kibongo
 |
| Athumani Lali 'Budege' |
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi Lali amesema kuwa kwa sasa yupo katika atua
za mwisho kwa ajili ya kutoa filamu mpya inayokwenda kwa jina la Faza
Hausi ambayo imeshilikisha wasanii wakongwe ndani yake akiwemo Mohamed
Nurdini 'Chekbudi' ,Esha Buheti, Rashidi Mwishehe 'Kingwendu' Muogo
Mchungu .
Filamu
hiyo itakayo tolewa na Kampuni hiyo ya jijini Dar es salaam itakuwa
moto wa kuotea mbali kwani si ya kukosa kabisa kwa mashabiki wa filamu
nchini.
filamu
hiyo ya Faza Hausi itakuwa mtaani wakati wowote kuanzia sasa kwani
takribani vitu vyote muhimu vimeshafanyika hivyo wadau wakae mkao wa
kula kwani filamu hii si yakuikosa
Ambapo itapatikana Tanzania nzima nikianzia Dar es salaam na mikoa yote filamu hiyo itawafikia
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi