MWANAUME mmoja aliuawa na wanakijiji muda
mchache tu baada ya kumuua babake kwenye kisa ambacho kiliwashangaza
wakazi wa kaunti ya Nyamira.
Mshukiwa
huyo, Bw Nyairo Nyaenya, 26 alimdunga kisu babake Bw Joseck Nyaenya
Orobi, 60 naibu wa kamati ya kudumisha usalama vijijini (Community
Policing) katika kijiji cha Omwaro na kumuua papo hapo.
Mshukiwa huyo
baadaye alijifungia ndani ya nyumba yake na mwanawe wa kiume wa miaka
kumi na kutisha kumuua kama yeyote angemfuata huko na kujaribu kumdhuru.
Lakini mama
wa mshukiwa huyo Bi Yusavia Nyaenya alipiga nduru na wanakijiji
waliofika hapo walivunja na kuingia ndani ya nyumba na kumuua mshukiwa
huyo na kumuokoa mtoto aliyekuwa ametekwa nyara.
Kitu cha
kushangaza ni kuwa wanakijiji hao walitaka kumuua pia mtoto huyo
waliyemuokoa wakisema hawakuwa wanataka kizazi cha mshukiwa huyo
kiendelee kwa sababu ya vituko vingi alivyokuwa ametenda katika kijiji
hicho.
Lakini kwa
bahati nzuri kamanda mkuu wa kituo cha polisi cha Nyamira Bw David
Muange na naibu wa chifu wa kata ndogo ya Bigege Bw Justus Okenye
waliokuwa wamefika mahali hapo walimwokoa mtoto huyo.
Damu ya mbwa
Kabla ya Bw Nyairo kumuua babake, alichinja mbwa na kunywa damu yake, kisa ambacho kiliwashangaza babake na mamake.
Pia alikatakata migomba kwenye shamba la familia hiyo.
Bw Okenye alisema taharuki ilitanda waaakati Bw Orobi alijaribu kujua ni kwa nini Bw Nyairo alikuwa na tabia isiyoleweka.
“Nyairo
ambaye alikuwa amejihami kwa panga na kisu alianza kumkimbiza babake.
Kwa bahati mbaya mzee huyo alianguka na kuawa hapo hapo,” Bw Okenye
alisema.
Alisema hivi karibuni, Bw Nyairo alikuwa ameua ng’ombe wao bila sababu yoyote.
“Mkewe mshukiwa huyo aliachana naye kwa sababu ya tabia yake isiyoeleweka,” Bw Oknye alisema.
Kis hicho
kilitendeka katika bkata ya Bosamaro Chache kwenye eneobunge la
Mugirango Magharibi kiliwashangaza wakazi wa eneo hilo.
Miili wa wawili hao ilipelekwa katika mochari ya hospitali kuu ya Nyamira.
