skip to main |
skip to sidebar
WENGI WATAKA KUJIUNGA NA KANISA LA WALA NYASI
Na Mwandishi Wetu
BAADHI ya wananchi jijini Dar wamejitokeza na kuomba kujiunga na kanisa ambalo waumini wake wanakula nyasi.
Waumini wakila nyasi.
Kanisa hilo ambalo makao yake makuu ni Afrika Kusini linaloitwa
Rabboni Centre Ministries gazeti hili liliandika katika toleo lake
lililopita kuwa limeingia nchini na lipo maeneo ya Upanga jijini Dar.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili mara baada ya kusoma habari hiyo walisema wanatamani kujiunga.
“Mimi nataka kujiunga na kanisa hilo kwa sababu tunataka wokovu,” alisema mtu mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Amos.
Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Frida Mandade alisema ana hamu ya kujiunga na kanisa hilo kwa sababu zake binafsi.
Kanisa la Rabboni Centre Ministries lina makao yake makuu Pretoria
nchini Afrika Kusini na linaongozwa na mtu anayejiita Mchungaji na Nabii
Daniel Lesego ambaye alilianisha mwaka 2002.
Wakati
wa mfungo waumini wa kanisa hilo wametajwa kuwa huwa wanaishia kula
majani yaliyopo nje ya kanisa hilo kwa imani kuwa Roho Mtakatifu
huongoza mtu kula chochote manyasi hayo ni chakula kutoka mbinguni.
CHANZO: GPL
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi