Baadhi ya Wananchi ambao
hawajafanyiwa tohara, wametakiwa kuacha aibu na kujitokeza kwenye
vituo vya afya ili kuweza kupata huduma hiyo na kuacha kukwepa
kupata huduma katika vituo vyao ambavyo wamevizoea.
Hayo yamesemwa na
meneja wa Mradi wa tohara mkoa wa iringa Dr.Abdalah Maganga, na kusema kuwa watu
kuanzia umri wa miaka 25 kwenda juu wamekuwa hawajitokezi kupatiwa huduma hiyo
kutokana na kuwa na aibu.
Dr.Abdalah amesema kuwa
asilimia kubwa ya watu wanaojitokeza kupata huduma hiyo ni wale wenye umri wa
miaka 18 kushuka chini ,huku sababu kubwa akitaja kuwa ni kuhofia kukaa muda
mrefu bila kufanya mapenzi kwa kipindi cha wiki sita wakati akisubiri kidonda
kupona.
Hata hivyo ametaja
sababu kubwa kuwa wengi wao hawapendi kufanyiwa tohara na wanawake kutokana na
kuwa idadi kubwa ya wahudumu ni wanawake.
Amesema kuwa katika
kampeni iliyofanyika katika kipindi cha wiki nne iliyolenga wilaya tatu imekuwa
na mafanikio ambapo mpango wao ilikuwa ni kuwafikia WATU 15 elfu lakini
wamefikia watu 16 elfu na 200 .
Aidha ameongeza
kuwa kuanzia tarehe 10 februali had 8 mach wataanza kampeni katika
wilaya za mkoa wa Njombe na lengo ni kuwafikia watu 15 elfu huku akiahidi
kurudia maeneo ambayo hawakuyafikia katika wilaya, ambazo tayari wamefanya
kampeni ambazo ni kilolo,iringa vijijini,na mufindi kwa wiki mbili.
