WAZAZI IRINGA WAASWA KUWAPELEKA WATOTO WAO SHULE KUTIMIZA HAKI YA MTOTO

Afisa elimu wa shule za sekondari Manispaa ya Iringa DEVOTA LONGO amewaasa  wazazi kuwapeleka watoto wao waliofanikiwa kujiunga na elimu ya shule za sekondari ili kutimiza haki ya mtoto.

Afisa elimu huyo pia amesema  atawachukulia hatua wazazi ambao hawatafanya agizo hilo.  
amesema kuwa kumewekwa mipango madhubuti ya kukabiliana na wazazi wote ambao hawatawapeleka watoto wao mashuleni ikiwemo kuongea na maafisa watendaji ili kuwapa idadi ya wazazi ambao hawajawapeleka watoto mashuleni pamoja na kuwafikisha polisi.

Hata hivyo amewaomba watendaji wa kata kupitia shule zilizopo katika kata zao ili kuhakikisha wanafunzi waliofanikiwa kujiunga na kidato cha pili wamewasili mashuleni.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo