skip to main |
skip to sidebar
WATATU KIZIMBANI KWA WIZI WA RECEIVER YA MAMILIONI YA FEDHA MALI YA SEKONDARI KIFANYA NJOMBE
Wakazi Watatu
wa Kijiji cha Kifanya Wilayani Njombe Maurus Chengula, Victorn Yordan
Maarufu Kwa Jina la Mayemba na Raymond Chengula Wamefikishwa Katika
Mahakama ya Wilaya ya Njombe na Kusomewa Shtaka la Wizi wa GPS Receiver
Yenye Thamani ya Zaidi ya Shilingi Milioni 16 Mali ya Shule ya Sekondari
Kifanya.
Akisoma Hati ya Mashtaka Mbele ya Hakimu wa Mahakama
Hiyo John Kapokolo, Mwendesha Mashtaka Wakili wa Serikali Yahaya Misango
Ameiambi Mahakama Kuwa Washtakiwa Hao Ambao ni Walinzi wa Shule Hiyo
Walitenda Kosa Hilo Januari Sita Mwaka Huu.
Hata Hivyo
Washtakaiwa Walipohojiwa Kuhusika na Kosa Hilo Wamekana , Huku Mwendesha
Mashtaka Wakili Huyo wa Serikali Akiiambia Mahakama Kuwa Upelele Juu ya
Wizi Huo Bado Unaendelea .
Hakimu
wa Mahakama Hiyo John Kapokolo Ameahirisha Kesi Hiyo Hadi Februari Nne
Mwaka Huu Kesi Hiyo Itakaposikilizwa Mara Baada ya Upelelezi Kukamilika
Huku Akisema Dhamana Kwa Washtakiwa Iko Wazi.
Na Gabriel Kilamlya
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi