Habari zilizoufikia zinasema kuwa Wanafunzi wanne Wa
shule ya sekondari Mustapha Sabodo iliyopo mjini Mtwara wamekufa na wengine
zaidi ya 20 kujeruhiwa baada ya kugongwa na gari aina ya Benz wakiwa
kwenye mchakamchaka asubuhi ya leo.
Chanzo cha ajali hiyo kinatokana na gari dogo aina ya Benzi
kumgonga mwanafunzi mmoja aliyekuwa kwenye mchakamchaka na katika hali ya
taharuki ya mwenzao bila kuangalia nyuma ndipo lori jingine likawagonga wanafunzi wengine na
kusababisha mwanafunzi mmoja kufariki dunia papo hapo na wengine watatu
wakifariki hospitali wakati wakipatiwa matibabu huku wengine 20 wakiwa wamejeruhiwa.
Dreva wa Benzi amejisalimisha kituo cha polisi Mtwara lakini
Yule wa Lori amekimbia.