Marehemu Tryphone Mpiluka enzi za uhai wake akitangaza redio Kitulo FM
Tasnia ya habari imepata pigo baada ya mwanahabari aliyekuwa akiendelea na masomo yake ya uandishi wa habari Bw. Tryphone Mpiluka kufariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo kwa ajali
Taarifa za awali zinasema Marehemu Tryphone amepoteza maisha baada ya kugongwa na gari wakati akisafiri kuelekea shambani kwa kutumia baiskeli hali iliyopelekea kifo chake huko Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa
Enzi za uhai wake marehemu alifahamika sana nyanda za juu kusini hasa wilayani Makete na maeneo ya jirani wakati akifanya mazoezi ya utangazaji katika kituo cha redio Kitulo FM kinachomilikiwa na halmashauri ya wilaya ya Makete
Kutokana na umahiri wake wa kutangaza marehemu aliamua kuendelea zaidi na masomo ambapo hadi mauti yanamkuta alikuwa akisoma masomo ya uandishi wa habari na utangazaji katika chuo cha Royal College Of Tanzania
Mungu aiweke roho ya marehemu Tryphone Mpiluka mahali pema peponi Amen
zifuatazo ni baadhi ya picha za marehemu enzi za uhai wake


