MWAIKIMBA KUTOKA AZAM FC ANUNUA GARI LA MILIONI 18, LITAZAME HAPA

Martha Mboma na Musa Mateja
MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Gaudence Mwaikimba, amefanikiwa kupiga hatua baada ya hivi karibuni kununua gari aina ya Toyota Brevis lenye thamani ya shilingi milioni 18.

Championi lilimshuhudia Mwaikimba aliyewahi kukipiga Yanga miaka ya nyuma akiwa na ndinga yake hiyo alipokuwa akihudhuria kwenye mazoezi ya timu hiyo yanayofanyika kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar, juzi.

Mwaikimba anayesadikika kuwa mrefu kuliko wachezaji wengine klabuni hapo, alisema kuwa aliupenda muundo wa gari hilo ulivyo ndiyo maana akaamua kulinunua kwa ajili ya matumizi yake na familia.

“Nafurahi na najivunia kuwa na aina ya gari hii ya Brevis kwa sababu ni matunda ya kazi yangu na nimenunua shilingi milioni 18, kujituma kwangu na kujiwajibisha kumenisaidia sana kufikia hapa nilipo.

“Japo si gari yangu ya kwanza kumiliki, nilishawahi kumiliki magari ya aina tofauti sana na baada ya kuwa namiliki ile Baloon ya kipindi kile ambacho nilikuwa nacheza Yanga, niliiuza na kununua nyingine, japo ilikuwa inapendwa na wengi kutokana na mbwembwe zake lakini kwa sasa ndiyo namiliki hii Brevis,” alisema Mwaikimba.

VIA GPL


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo