Taarifa kutoka hapa mahakama kuu Dar ni kwamba Zitto Kabwe ameshinda kesi dhidi ya Chadema, wafuasi wa Zitto wamejawa na furaha kupita kiasi
Kwa mantiki hiyo Zitto amepewa kinga na mahakama hiyo hivyo Chadema haitamjadili
Ikumbukwe kuwa LEO macho na maskio ya watanzania hasa wafuasi na wapenzi wa CHADEMA yalielekezwa katika Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es Salaam,pale ambapo Jaji wa Mahakama hiyo Jaji John
Utumwa alikuwa akitoa hukumu dhidi ya Zitto Kabwe na CHADEMA....
Zitto ambaye alikuwa ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, alifungua kesi
katika Mahakama hiyo akipinga hatua ya Kamati Kuu ya Chama hicho iliyokutana tarehe 3 na 4 mwezi huu
kujadili hatima ya uanachama wake wakati baraza kuu halijakaa na kujadili rufaa yake...
Akisoma hukumu ya kesi hiyo baada ya kuiahirisha jana, Jaji wa mahakama hiyo,Jaji
Utamwa ameridhia pingamizi lililotolewa na mh. Zitto Kabwe la
kutojadili uanachama wake na kuitaka kamati kuu ya CHADEMA au
chombo kingine chochote kisijadili uanachama wake hadi kesi
yake ya msingi ( rufaa ) itakaposikilizwa na baraza kuu la
chama hicho.