Waziri wa uchukuzi Mheshimiwa daktari Harrison Mwakyembe amesema
hatua kubwa ya ujenzi wa barabara za lami umeingiza Tanzania katika
matatizo makubwa kutokana na zaidi ya asilimia 95 ya mizigo
inayosafirishwa mikoani na nchi jirani kutumia usafiri wa barabara
badala ya reli hali inayohatarisha ubora wa barabara hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano
wa kimataifa wa nchi za bonde la ufa unaojadili miundombinu na uchukuzi
kwa upande wa mashariki, kusini na Afrika ya kati, daktari Mwakyembe
matumizi ya reli ndio njia mbadala ya kulinda ubora barabara na
kusisitiza tatizo lililopo sekta binafsi inashindwa kuwekeza katika reli
kutokana na kuhitaji gharama kubwa na idadi kubwa ya mabenki
yanamasharti magumu.
Awali akielezea changamoto za uchukuzi katika
ukanda wa kati,mtaalamu wa miundombinu kutoka mamlaka ya uwezeshaji wa
uchukuzi kanda ya kati-TTFA- mhandisi Charles Sabiti ameainisha
changamoto zinazoikabili sekta ya uchukuzi katika ukanda huo zikiwemo
mfumo mbovu wa reli,kutokuwepo kwa viwango sawa vya vipimo vya uzito wa
mizigo pamoja na ucheleweshwaji wa nyaraka sahihi za waingiza mizigo.
Kwa upande wake meneja mradi kutoka shirika la
entico ambao ndio waandaji wa mkutano huo,bwana Warren Ersen amesema
lengo la mkutano huo ni kuwawezesha washiriki kutoka zaidi ya nchi 12
kubadilishana uzoefu wa namna ya kukabiliana na changamoto za
miundombinu na kuongeza na wawekezaji,ambapo amesisitiza hakuna
uwezekano wa kuboresha sekta ya uchukuzi kwa kipindi kifupi na
kusisitiza inachukua zaidi ya miaka 6 matokeo yake usaidia kushusha
gharama za bidhaa kwa watumiaji kutokana na unafuu wa usafirishaji.