UKATILI MKUBWA: WATOTO WAWILI WACHOMWA MOTO VIGANJA VYAO VYA MIKONO NA BABA YAO

Watoto wawili wenye umri wa miaka tisa,wamechomwa moto viganja vyao vya mikono na baba zao katika wilaya ya Newala mkoani Mtwara.

Ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku kumi na sita za kupinga ukatili wa kijinsia hapa nchini, ITV kwa kushirikiana na chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA waliamua kufuatilia tukio la ukatili waliofanyiwa watoto hao kwa kuchomwa moto viganja vya mikono yao na baba zao walowazaa kwa kumtafuta kwanza afisa ustawi wa jamii wa wilaya ya Newala bwana George Martin Shinganya ili kueleza walichofanyiwa watoto hao katika vijiji tofauti vya wilaya hiyo.

ITV ililazimika kumtafuta mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mwongozo katika kijiji cha Makonga kata ya Nambunga bwana Nurdin Machemba,na kueleza kuwa alishughulikia suala la mtoto huyo kama mwanafunzi wake na kisha kukabidhi uongozi wa serikali ya kijiji kuendelea nayo lakini mtuhumiwa amekimbilia nchi ya Msumbiji hivyo kuomba serikali kusaidia ili akamatwe.

chanzo:ITV


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo