MTU MMOJA AGONGWA NA FUSO NA KUSAGIKA MIGUU NJIA PANDA KIA MKOANI KILIMANJARO..ONYO! PICHA HIZI ZA AJALI ZINATISHA



MZEE huyu wa jamii ya kabila la wamasai aliyetambulika kwa jina la ''Tulito'' Mkaazi wa KIA njia panda ya kuelekea uwanja wa ndege wa Kilimanjaro International Airpot, Leo mda mfupi uliopita amepata ajali mbaya ya kugongwa na fuso alipofanya jaribio la kuvuka barabara hio ya lami ambayo magari huenda mwendo kasi, Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka mkoni kilimanjaro kimedai kwamba gari hilo aina ya FUSO halikusimama baada ya kumgonja mzee Tulito lilitokomea..! Raia waliokuwa karibu na eneo la tukio hawakufanikiwa kunasa walau hata namba za gari hilo, Mzee tulito aliwahishwa Hospitali wilayani boma kwa matibabu zaidi. 
Imeripotiwa na Afande wa Ust taifa (Dj Tindo)










Hapa mzee Tulito akipakiwa kwenye gari kuwahishwa Hospitali wilayani Boma ya Ng'ombe Mkoani Kilimanjaro.

MTANDAO HUU Unamuombea mzee Tulito apone haraka akaendelee na maisha mema na familia yake.
 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo