Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akitoaa taarifa ya shule hiyo kwa katibu mkuu wa CCM na Ujumbe wake
Saruji kwa ajili ya ujenzi ikiteremshwa kwenye lori
Madarasa yakisubiri wanafunzi
Viongozi wa wilaya wakiongozwa na mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro( wa pili kushoto) wakiangalia mafundi wakichimba msingi wa bweni.
====
Juhudi zinazofanywa na mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro kurahisisha upatikanaji wa elimu wilayani mwake zinazidi kung'ara baada ya neema kuishukia shule ya sekondari ya wasichana iliyopo kijiji cha Utweve kata ya Ukwama na kuacha raha kwa wananchi walioshuhudia neema hiyo
Hiyo ni kufuatia viongozi wakuu wa chama cha mapinduzi (CCM) taifa wakiongozwa na katibu wao Ndugu Abdulrahman Kinana kutembelea shule hiyo ambayo bado inaendelea kujengwa na kuahidi mbele ya hadhara iliyohuduria kuwa CCM Taifa itatoa mabati 200 kwa ajili ya ujenzi katika shule hiyo
Katibu mkuu Ndg Kinana ndiye aliyetoa ahadi hiyo mara baada ya kujionea nguvu za wananchi, mfuko wa maeendeleo ya jamii TASAF na halmashauri ya wilaya ya Makete kuunganisha nguvu zao na kufanikiwa kujenga vyumba vitatu vya madarasa, nyumba ya mwalimu pamoja na vyoo
Awali akitoa maelezo mafupi kuhusu shule hiyo, mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro amesema shule hiyo ni ya kwanza wilayani hapo kuwa na wanafunzi wasichana pekee, hivyo wanatarajia kuanza kupokea wanafunzi Januari mwakani
Amesema kwa sasa wanajenga hosteli kwa ajili ya wanafunzi hao, ila kwa kuanzia watatumia chumba kimoja cha darasa kama hosteli wakati ujenzi wa bweni ukiendelea, huku akiomba kusaidiwa bati 200 kwa ajili ya shule hiyo, ambazo zitatolewa na CCM kwa ahadi ya katibu mkuu wa CCM
Mtandao huu umeshuhudia vifaa vya ujenzi vikishushwa shuleni hapo ikiwemo mifuko 100 ya saruji, na mafundi wakiendelea kuchimba msingi wa mabweni hayo
Matiro amesema ujenzi wa shule hiyo ni utekelezaji wa ilani ya CCM yenye kutaka kuhakikisha elimu inawafikia wanafunzi wote wanaotakiwa kuipata bila kujali itikadi ya kitu chochote, na kuongeza kuwa ushirikiano alioupata kutoka kwa wakazi wa makete ambao wanakaa nje ya wilaya hiyo, kwani nao wanashiriki kwa pamoja na serikali na wadau wote kuhakikisha shule hiyo inakamilika