BASI LA KWANZA LA MRADI WA MABASI YAENDAYO KASI LAANZA KAZI JIJINI DAR




Mabasi ya mwendo kasi 2014 kimara kivukoni.  Picha kwa hisani ya Deo Mutta Mwanatanga
Basi la kwanza la mradi wa mabasi yaendayo haraka limewasili nchini na kuanza kufanya majaribio katika barabara zilizokwisha kamilika huku mengine yakitarajiwa kuwasili mapema mwaka kesho.
Mtendaji mkuu wakala wa mradi wa mabasi yaendayo haraka Bi Asteria lambo amesema basi hilo ni miongoni mwa mabasi madogo yatakayoingia nchini yenye uwezo wa kubeba zaidi ya abiria 40 na makubwa yatabeba abiria zaidi ya 150 na kuwataka wakazi wa jiji la Dar es Salamu kuendelea kuwa na subira na kuwahakikishia mradi huo sio ndoto na adha ya usafiri itapungua mapema mwaka kesho.
Nao baadhi ya wakazi wa jiji walioshuhudia gari hilo wameelezea kufurahishwa na kuanza kuwa na imani na serikali yao ambapo wamesema kama mradi huo utakamilika kwa muda uliopangwa utakuwa faraja sana kutokana na adha kubwa ya usafiri wanayokumbana nayo  huku wakitoa wito kwa mamlaka husika kupanga mikakati ya kupunguza nauli za mabasi hayo pindi yatakapoanza kufanya safari zao.
ITV


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo