Serikali
imewataka wananchi wenye uhitaji wa elimu ya watu wazima kuchangamkia
fursa ya kujitokeza katika kujiunga na mfumo wa elimu hiyo ili
kujiendeleza na kuinua kiwango cha elimu nchini na kwa taifa kwa ujumla.
Mkuu wa wilaya ya Ilala Raymond Mushi akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam katika kilele cha maadhimisho ya siku ya elimu ya watu wazima kwa mkoa wa Dar es salaam amesema dhamira ya serikali ni kuhakikisha kuwa mifumo yote miwili yaani ulio rasmi na usio rasmi inajikita katika kumuondolea umasikini Mtanzania na kumsaidia kujikwamua kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni.
Aidha bwana Mushi amesema mfumo wa elimu hiyo pia unatolewa ndani ya magereza kwa wafungwa wa umri mbalimbali na jinsia tofauti tofauti lengo likiwa kuwapatia mafunzo wafungwa ili waweze kujiendeleza na elimu nyinginezo punde wanapomaliza adhabu ya vifungo vyao.