
Na Prosper Mfugale Njombe
Zaidi ya Wateja Mia Sita wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Wilayani Njombe Wameulalamikia Uongozi wa Shirika Hilo Kwa Kushindwa Kuwaunganishia Huduma ya Umeme Kwa Zaidi ya Miezi Sita Licha ya Kukamilisha Taratibu Zote Ikiwemo Malipo ya Huduma Hiyo.
Aidha Wateja Hao Wamelalamikia Kitendo Cha Shirika Hilo Kukiuka Mkataba wa Huduma Kwa Mteja Ambao Kwa Mujibu wa Wateja Hao Walitakiwa Kuunganishiwa Huduma Hiyo Ndani ya Siku Thelathini Baada ya Kukamilisha Malipo na Kujaza Mkataba.
Wakizungumza na mwandishi wa mtandao huu Baadhi ya Wateja Hao Wamesema Licha ya Kufika Mara Kadhaa Katika Ofisi za Shirika Hilo Kwaajili ya Kufuatilia,Bado Kumekuwa Hakuna Majibu ya Uhakika Jambo Linalosababisha Kushindwa Kupata Huduma Hiyo Hadi Sasa.
Akizungumzia Hali Hiyo Meneja wa TANESCO Wilaya ya Njombe Mhandisi Emanuel Kachewa Amesema Tatizo Hilo Limetokana na Upungufu wa Vifaa Unaolikabili Shirika Hilo Kwasasa na Kusema Hali Hiyo Imeendelea Kujitokeza Katika Mikoa Mbalimbali Nchini.
Kutokana na Hali Hiyo Bw Kachewa Amewataka Wateja Hao Kuendelea Wavumilivu Katika Kipindi Hiki Ambapo Shirika Hilo Linaendelea Kulitafutia Ufumbuzi Tatizo Hilo na Kuongeza Kuwa Tayari Shirika Hilo
Limezungumza na Wateja Hao na Kuwafahamisha Tatizo Lililopo Kwasasa.