Waziri
Mkuu alieyejiuzulu ambae pia ni Mbunge wa Monduli CCM,Edward
Lowasa,(kushoto) wakifurahia jambo wakati wa mazungumzo yao na
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions,Alex Msama, walipokutana nje
ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma,mara baada ya kuahirishwa kwa kipindi
cha maswali na majibu.
Waziri
wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera uratibu na bunge,William
Lukuvi(kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama
Promotions,Alex Msama(kulia) walipokuwa wakizungumza jambo.
Mbunge
wa Msalala,CCM,Ezekiel Maige,(katikati) wakibadilishana mawazo kuhusu
changamoto mbalimbali za kisiasa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama
Promotions,Alex Msama walipokutana kwenye viwanja vya bunge mjini
Dodoma,(kushoto) ni Mbunge wa Kigoma kusini David Kafulila.
Waziri
wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka(kushoto)
akifurahia kukutana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions,Alex
Msama,nje ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma,, (katikati)ni Naibu Waziri wa wizara hiyo
Gudluck Ole Medeye.
Spika
wa Bunge Anne Makinda,(kulia)akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa
Kampuni ya Msama Promotions,Alex Msama (kushoto) alipotembelea bungeni
ili kukutana na viongozi mbali mbali wa vyama vya siasa na Serikali.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala bora, George Mkuchika(kushoto)akiagana
kwa msisitizo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions,Alex
Msama(kulia).Msama ambae ni mdau mkubwa wa mambo ya siasa na Muziki wa
Injili alitembelea bungeni mjini Dodoma ili kukutana na viongozi wa
Vyama vya siasa na Serikali,bunge linaendelea na vikao vyake.