BALOZI SEIF IDDI AZIASA REDIO ZA JAMII KUWA CHACHU YA MAENDELEO VISIWANI ZANZIBAR

IMG_2464
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na wananchi wa Kisiwa cha Tumbatu katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Matangazo ya Redio Jamii Kisiwani humo.

Na. Othman Khamis Ame

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Vituo vya Redio Jamii hapa Nchini vinapaswa kuwa chem Chem ya elimu itakayotoa manufaa kwa Jamii inayovizunguuka Vituo hivyo badala ya utaratibu wa kurusha vipindi vya muziki wakati wote.

Kauli hiyo aliitoa wakati akiizindua Redio Jamii ya Wilaya ndogo ya Tumbatu hapo katika jengo la Wilaya hiyo liliopo katika Kijiji cha Kichangani ikiwa ni muendelezo wa shamra shamra za maadhimisho ya kutimia miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.

Balozi Seif alisema mijadala na nakala zinazohusiana na masuala ya Uchumi, siasa, jamii na Maendeleo ndio lengo lililokusudiwa katika uanzishwaji wa Redio hizo na kupelekea kuungwa mkono na Taasisi na mashirika ya maendeleo Duniani.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwataka watendaji wa Redio Jamii Tumbatu kujitahidi kuwaelimisha wananchi kuhusu uvuvi bora na mambo mengi yanayohusiana na bahari kwani maisha ya wananchi hao yametegemea zaidi sekta ya bahari.
IMG_2183
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikata utepe kuzindua rasmi Redio Jamii ya Wilaya ndogo ya Tumbatu visiwani Zanzibar. Kushoto ni Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Elimu, Sayansi na Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa (Unesco)Bw. Abdul Wahab Coulibaly wanaofadhili unzishwaji wa redio za jamii Tanzania Bara na Visiwani.
116
Mkurugenzi wa Kituo cha Redio Jamii cha Tumbatu Ali Khamis Mtwana akimpatia maelezo juu ya utendaji wa Kituo hicho Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya kukizindua rasmi.
Kulia kwa Balozi Seif ni Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Unesco Bw. Abdul Wahab Coulibaly na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali Mbaouk.
123
Mkurugenzi wa Kituo cha Redio Jamii cha Tumbatu Ali Khamis Mtwana akifanya vitu vyake wakati akiwa hewani kurusha matangazo ya kituo cha Redio Jamii Tumbatu mara baada ya kuzinduliwa na Balozi Seif Ali Iddi. Kushoto kwa Balozi Sefu ni Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Elimu, Sayansi na Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa (Unesco)Bw. Abdul Wahab Coulibaly wafadhili wa mradi huo.(Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ na Zainul Mzige wa MOblog).


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo